Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) –ABNA– Ayatollah Sayyid Muhammad Taqi Modarresi, mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu nchini Iraq, ameeleza kuwa elimu ndiyo njia pekee ya maendeleo ya mataifa na kufikia viwango vya juu vya mafanikio, huku akiwahimiza wanafunzi wa seminari za kidini (Hawza) kujifunza historia na maisha ya wanazuoni wema na kufuata mifano yao.
Ayatollah Modarresi amesisitiza umuhimu wa elimu katika kuendeleza jamii na kuinua hadhi ya mataifa, akieleza kuwa mafanikio na kufikia viwango vya juu kunategemea kujituma katika kutafuta elimu na kuiga mwenendo wa watu waliotangulia ambao walijipambanua kwa elimu, uchamungu na maadili mema.
Aidha, amewahimiza wanafunzi wa Hawza kutafakari maisha ya wanazuoni wema, kujifunza kutokana na juhudi, mwenendo na mafanikio yao, na kuyafanya kuwa mwongozo katika safari yao ya kielimu na kiroho.
Maoni yako